Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 00:42

Benki za biashara Afrika Mashariki zakabiliwa na mikopo isiyolipika


Ramani ya Afrika Mashariki
Ramani ya Afrika Mashariki

Benki za biashara Afrika Mashariki zimerekodi zaidi ya dola milioni 125 ya mikopo isiyolipika katika kipindi cha miezi tisa kufikia Septemba mwaka 2021.

Wakati huu wakopaji wanaendelea kuhangaika kulipa mikopo yao baada ya muda wa miezi 12 ya programu yenye unafuu wa kulipa mikopo hiyo kwa wateja walioathirika na janga la COVID-19 kumalizika.

Hili limekuja wakati wadhibiti wa mabenki nchini Kenya, Tanzania na Rwanda wakielezea wasiwasi wao juu ya kuongezeka kwa madeni yasiyolipika, ambayo hivi sasa yanatishia sekta hiyo ya fedha.

Wiki iliyopita, Benki Kuu ya Rwanda ilirejesha masharti yaliyotaka kwa benki za biashara kuongeza upatikanaji wa mikopo iliyokuwa imesitishwa kutokana na janga hilo kuziwezesha benki kuendelea kukopesha. Kurejeshwa huko kunaweza kuathiri mikopo kwa sekta binafsi

Wakati huohuo Benki Kuu ya Tanzania imeanzisha hatua za kukabiliana na mikopo isiyolipika, ikiwemo kuwajumuisha wafanyakazi wa benki ambao wanahusika moja kwa moja na utaoji wa mikopo hiyo.

Taarifa za karibuni za mahesabu ambazo hazijakaguliwa kuhusu wakopeshaji wa eneo, benki ya biashara ya KCB, Mabenki ya Equity and Cooperative zinaonyesha jumla ya kiwango cha mikopo isiyoweza kulipwa (NPLs) iliongezeka kwa asilimia nane kufikia dola bilioni 1.81, kutoka dola bilioni 1.68 katika kipindi hicho hicho mwaka 2020.

Co-operative bank ilikuwa na kiwango cha zaidi ya dola milioni 80.6 cha thamani ya mikopo iliyokuwa hailipiki katika kipindi cha tathmini, ikifuatiwa na Equity Bank iliyokuwa na dola milioni 39.46 na KCB yenye dola milioni 10.26 ya aina hiyo ya mikopo.

Kwa jumla, KCB ilikuwa na kiwango cha juu zaidi cha mikopo isiyolipika cha dola milioni 876.25, ikifuatiwa na mabenki ya Equity and Co-operative yenye dola milioni 501.6 na dola milioni 441.78.

XS
SM
MD
LG