Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:57

IMF yasema haina uwezo wa kuisaidia kifedha Zimbabwe


Shirika la Fedha Dunaini, IMF.
Shirika la Fedha Dunaini, IMF.

Shirika la Fedha Duniani, IMF, limesema halina uwezo wa kutoa msaada wowote wa kifedha kwa Zimbabwe kutokana na deni lake kubwa na kushindwa kulipa madeni yake.

IMF imesema kwamba wafanyakazi wake wamekamilisha mazungumzo yao kupitia mtandao na maafisa wa Zimbabwe kati ya Oktoba 16 na Novemba 16 na kubaini kwamba kuna haja kwa maafisa wa serikali ya Zimbabwe kukabiliana na mfumuko wa bei, kusawazisha bajeti yake na kuongeza akiba yake ya pesa.

Zimbabwe, ambayo imekumbana na mfumuko wa bei wa kiwango cha juu sana katika muda wa miaka 15 iliyopita, haijapata msaada wa kifedha kutoka kwa mashirika kama IMF na Benki ya Dunia, WB, kwa muda wa miongo miwili iliyopita.

Nchi hiyo inadaiwa zaidi ya dola bilioni 10.

Mwezi Septemba, serikali ilisema kwamba ilikuwa imepiga hatua kubwa katika kulipa madeni yake kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20.

Nchi hiyo ya kusini mwa Afrika imepitia kipindi kigumu cha uchumi kwa miaka mingi, sekta za viwanda na uuzaji wa bidhaa nje ya nchi zikikabiliwa na uhaba mkubwa, pamoja na ukosefu wa fedha za nje.

XS
SM
MD
LG