Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 18:24

Kampuni ya Google kuwekeza dola bilioni 1 Afrika


Ofisi ya Google karibu na makao makuu ya kampuni hiyo eneo la Mountain View, California, Marekani, Mei 82019. REUTERS/Paresh Dave/File Photo
Ofisi ya Google karibu na makao makuu ya kampuni hiyo eneo la Mountain View, California, Marekani, Mei 82019. REUTERS/Paresh Dave/File Photo

Kampuni ya Google imetangaza Jumatano uwekezaji wa dola bilioni moja kwa kipindi cha miaka mitano ijayo ili kuruhusu ukuaji wa haraka wa mtandao wa Internet na upatikanaji wake kirahisi na pia kusaidia wajasiriamali wa Afrika.

“Leo nina furaha kutangaza mpango wa kuwekeza dola bilioni moja Afrika kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitano. Itashugulikia juhudi kadhaa za kuboresha mungiliano wa uwekezaji. Uwekezaji huu utasaidia mabadiliko ya kidigitaji barani Afrika katika maeneo manne muhimu," kampuni hiyo imeeleza.

"Kwanza kuwezesha ufikiaji wa bidhaa za ujenzi kwa kila mtumiaji wa kiafrika. Pili kusaidia biashara na mabadiliko yao ya digitali. Tatu, kuwekeza kwa wajasiriamali ili kukuza teknolojia za kizazi kijacho. Na nne kusaidia mashirika yasio ya faida yanayofanya kazi kuboresha Maisha kote Afrika,” imeongeza

Ramani ya Africa
Ramani ya Africa

Kutegemea internet ni tatizo katika bara la Afrika ambapo chini ya theluthi moja ya watu bilioni 1.3 wa bara hilo wameunganishwa katika mtandao, hiyo ni kwa mujibu wa benki ya dunia.

Lakini katika bara hilo ambapo karibu nusu ya idadi ya watu ni chini ya miaka 18 ndiyo soko la internet .

XS
SM
MD
LG