Makabidhiano hayo yamefanyika Ikulu jijini Dar es salaam na ujumbe Maalum kutoka Kenya ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Monica Juma
Rais John Magufuli alipokuwa anapokea kilo 35 za dhahabu hiyo ameishukuru Serikali ya Kenya chini ya Rais Uhuru Kenyatta kwa kukubali ombi la Serikali ya Tanzania.
Serikali ilikuwa imeiomba serikali ya Kenya kurudisha dhahabu hiyo sambamba na watuhumiwa wa utoroshaji huo ili kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa Rais Magufuli alimpigia simu Rais Kenyata ambaye ambaye alimhakikisha azma yao ya kuhakikisha maliasili za mataiafa hayo miwili zinabaki kuwanufaisha wananchi wao, hivyo vitendo vya kuhujumu havitavumiliwa.
Vipande hivyo 22 vya dhahabu vilikamatwa Februari mwaka 2018, katika Uwanja wa ndege wa kimataiafa wa Jomo Kenyatta wakati fedha taslimu zaidi ya milioni 500 zilikamatwa mwaka 2004 na vyote vimerudishwa na vitatumika kama ushahidi katika kesi ya wahalifu hao.
Imetayarishwa na mwandishi wetu Washington, DC.