Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 07:42

Kashfa ya Reagan kuwaita Waafrika nyani yaibuka kutoka maktaba ya Nixon


Ronald Reagan wakati huo gavana wa jimbo la California akizungumza katika mkutano wa chama cha Republican,1972.
Ronald Reagan wakati huo gavana wa jimbo la California akizungumza katika mkutano wa chama cha Republican,1972.

Kanda mpya za sauti zilizopatikana katika maktaba ya kumbukumbu ya rais wa zamani Richard Nixon zimefichua mazungumzo ambapo rais mwingine wa zamani Ronald Reagan aliwaita waafrika “nyani” katika mazungumzo yao ya simu.

Mazungumzo hayo yaliyotokea mwaka 1971 baada ya Umoja wa Mataifa kupiga kura ya kuiingiza China katika umoja huo ikiongozwa na Tanzania ambapo ujumbe wa nchi hiyo ulionekana ukicheza kwa furaha katika ukumbi wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa. Aliyekuwa Balozi wa Tanzania katika umoja huo Salim Ahmed Salim ndio aliyeongoza ujumbe wa Tanzania.

Katika mazungumzo ya simu baina ya Reagan na rais Nixon, wakati huo Reagan akiwa Gavana wa California alisikika akisema “kuwaona nyani wale kutoka nchi za afrika – (tusi) hata bado hawawezi kuvaa viatu."

Sauti hiyo iliyokuwa haijawahi kutolewa imeibuliwa wiki kadhaa baada ya Rais Donald Trump kutumia lugha ya kibaguzi kuwashambulia wanawake wanne wa chama cha Demokrat wenye asili za mchanganyiko, akikusudia wao siyo Wamarekani halisi na kupendekeza “warejee makwao na kusaidia kutatua maeneo yao wanakotokea yaliyokuwa yameghubikwa na uhalifu

Tim Naftali, aliyekuwa anasimamia maktaba ya rais Richard Nixon na Makumbusho kuanzia 2007 hadi 2011, ameandika kuwa Reagan – ambaye baadae alikuja kuwa Rais wa 40 wa Marekani – alimpigia simu Nixon Octoba 1971, siku moja baada ya Umoja wa Mataifa kupiga kura kuitambua Jamhuri ya Watu wa China.

Katika mazungumzo yake hayo, anasema, Reagan alisikika kwa namna fulani akieleza jinsi ujumbe wa Tanzania ulivyoanza kucheza ngoma katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati kura ya kuruhusu ujumbe kutoka Beijing kuingia uanachama badala ya Taiwan.

Reagan, anaandika Naftali, anasikika akimwambia Nixon, “Jana usiku, nakwambia, kuangalia tukio hilo kupitia televisheni kama nilivyoona.”

Nixon amkatiza : “Ndio.”

Reagan akaendelea kusema, “Kuona watu hao, hao manyani kutoka nchi hizo za Afrika – walaaniwe, wanaonekana hawana mazoea ya kuvaa viatu!”

Reagan – ambaye ni mtetezi wa dhati wa Taiwan aliyekuwa anaukashifu Umoja Mataifa – alikuwa anataka Marekani ijiondoe kushiriki kikamilifu, Naftali alisema.

Ofisi ya Kumbukumbu ya Taifa awali ilitoa kanda yenye mazungumzo ya simu mwaka 2000 bila ya kipande chenye ubaguzi, lakini kama mtafiti, Naftali amesema, aliomba mazungumzo hayo ya Nixon na Reagan yasikilizwe upya mwaka 2018.

Ofisi hiyo ilitoa mazungumzo hayo kamili ya rikodi hiyo mtandaoni wiki mbili zilizopita.

Katika rikodi nyingine, Naftali anaandika, Nixon baadae alimpigia simu aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje William Rogers na kurejea mazungumzo yale yale aliyofanya na Reagan.

“Kama unavyoweza kufikiria,” Nixon alimwambia Rogers, “kuna hisia kali kuwa tusifanye hilo, kama Reagan alivyosema, aliona haya… wanyama kwenye televisheni jana usiku, na anasema, ‘Yesu, hawakuwa hata wamevaa viatu, na hapa Marekani itatoa hatma yake juu ya hilo,’ na mengine kadha wa kadha.”

XS
SM
MD
LG