Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 16:52

AU yamtaka Trump kuomba radhi


Rais Donald Trump akiwa katika mazungumzo na Bunge la Congress
Rais Donald Trump akiwa katika mazungumzo na Bunge la Congress

Umoja wa Afrika unasema matamshi yanayodaiwa kutolewa na Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu bara Afrika ni wazi kwamba ni kiashiria cha ubaguzi wa rangi.

Umoja wa Afrika umesema kuwa matamashi yanayodaiwa kuwa yalitolewa na Rais wa Marekani Donald Trump juu ya bara la Afrika yanaonyesha kuwa ni ubaguzi wa rangi. Kufuatia kauli hiyo AU imemtaka Rais Trump aombe radhi.

Vyanzo vya habari vimesema kuwa msemaji wa umoja huo, Ebba Kalondo, amesema tamko hilo lilikera zaidi hasa ikizingatiwa idadi ya Waafrika waliouzwa kama watumwa Marekani.

Hata hivyo Rais Trump alikanusha kuwa alitumia lugha chafu kuzielezea nchi za Afrika na Haiti wakati wa mkutano wake ikulu ya White House.

Vyombo vya Marekani viliripoti Alhamisi kuwa Trump alitoa tamko hilo wakati wa akizungumza juu ya sera ya uhamiaji ya Marekani inayojulikana kama DACA.

Kauli hiyo ilisema kuwa nchi hizo ni maskini zaidi na chafu. Kufuatia kauli hiyo AU imemtaka Rais Trump aombe radhi.

Uliongezea: Huku tukionyesha kushangazwa kwetu , Umoja wa Afrika unaamini pakubwa kwamba utawala mpya wa Marekani haulielewi bara la Afrika na watu wake.

''Kuna umuhimu mkubwa wa kuwepo kwa mazungumzo kati ya utawala wa Marekani na mataifa ya Afrika''.

Imeripotiwa kuwa Rais Trump alitoa matamshi hayo dhidi ya Africa, Haiti na Elsavador kwenye ikulu ya White house katika mkutano na wabunge wa congress.

Pia kwa mujibu wa Shirika la habari la BBC matamshi hayo yamekosolewa na wengi, likiwemo shirika la kimataifa kuhusu haki za binadamu.

XS
SM
MD
LG