Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 03:43

EU yasema mkataba wa nyuklia wa Iran imara


Wapinzani wa serikali ya Rais Hassan Rouhani wakiandamana nje ya jengo la Umoja wa Ulaya huko Brussels, Belgium Jan 03, 2018
Wapinzani wa serikali ya Rais Hassan Rouhani wakiandamana nje ya jengo la Umoja wa Ulaya huko Brussels, Belgium Jan 03, 2018

Mkuu wa masuala ya sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya (EU) amesema kuwa makubaliano ya kimataifa juu ya programu ya nyuklia ya Iran yana tija.

Amesema japokuwa kuna wasiwasi juu ya Iran kuendelea kutengeneza makombora ya balistika na harakati nyingine wanazofanya Mashariki ya Kati, masuala hayo yanafaa kushughulikiwa kama mambo ya kando.

Alizungumza hayo baada ya mkutano uliofanyika Alhamisi huko Brussels na mawaziri wa mambo ya nje wa Uingereza, Ujerumani na Iran kujadili mkataba wa 2015.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian amesema pande zote za mazungumzo ni lazima ziheshimu mkataba wa nyuklia, ikiwemo Marekani, ambayo ilikuwa ni sehemu ya washiriki wa mazungumzo hayo zikiwemo Uingereza, China, Russia na Ujerumani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Boris Johnson amesema ni muhimu kuweka “msimamo wa pamoja duniani” kwa ajili ya makubaliano hayo na kuwapa Iran nafasi ya kuonyesha kuwa “ ni jirani mwema.”

“... lakini kwa pamoja tujikite katika kuangalia kile ambacho Iran inaweza kufanya kutatua mgogoro wenye maafa makubwa nchini Yemen, kuwezesha mazungumzo ya amani Syria kusonga mbele na pia kusaidia masuala mengine katika eneo la Mashariki ya Kati,” amesema Johnson.

Ameongeza kuwa hafikirii kama kuna mtu yoyote ambaye amekuja na mpango mbadala bora zaidi juu ya makubaliano ya nyuklia ya Iran.

Rais Donald Trump anategemewa kufanya maamuzi Ijumaa iwapo aendelee kusitisha vikwazo ambavyo awali viliwekwa kuishinikiza Iran kuacha mara moja utengenezaji wa silaha za nyuklia.

Mkataba huo ulifikiwa kupitia azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kusimamiwa na Shirila la Kimataifa la Nguvu za Atomic, ambayo imethibitisha kuwa Iran inaendelea kuheshimu mkataba huo na kuwajibika ikiwemo kusitisha kurutubisha madini ya uranium na kuondoa mitambo yake.

XS
SM
MD
LG