Maafisa hao wanatakiwa kutoa maelezo kuhusiana na uchunguzi wa Russia unaoendelea juu ya nchi hiyo kuingilia kati uchaguzi wa rais Marekani mwaka 2016.
Pia kamati hiyo inaangalia hatua ya serikali ya Trump kutenganisha familia kwenye mpaka wa Marekani na Mexico.
Wademokrat, waliowengi katika baraza la wawakilishi wanaidhibithi kamati, waliwashinda kutokana na idadi ya kura zao na kumpa mamlaka mwenyekiti wa kamati hiyo Jerrold Nadler kutuma ujumbe wa kuwaita maafisa kadhaa wanaotumikia au waliokuwa karibu na rais Donald Trump kuja mbele ya kamati kuhojiwa.
Trump amelalamika mara kadhaa kwamba uchunguzi dhidi ya utawala wake ni njama tu za kumuwinda kisiasa.
Imetayarishwa na mwandishi wetu Washington, DC.