Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 22:05

Seneti Marekani yamwita mtoto wa Rais Trump kuhojiwa zaidi


Rais Donald Trump, kushoto, na mtoto wake Donald Trump Jr. (kulia)
Rais Donald Trump, kushoto, na mtoto wake Donald Trump Jr. (kulia)

Kamati ya Usalama ya Baraza la Seneti, Marekani, imemwita mtoto mkubwa wa Rais Donald Trump kujibu maswali juu ya ushahidi aliotoa mwaka 2017 kwa jopo hilo ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa kubaini iwapo Russia iliingilia kati uchaguzi.

Kamati hiyo imerejea upya nia yake ya kuzungumza na mtoto wa Donald Trump baada ya wakili wa zamani wa rais, Michael Cohen, alipoiambia kamati ya Baraza la Wawakilishi mwezi Februari kwamba alikuwa amemwarifu mtoto huyo takriban mara 10 juu ya mpango wa ujenzi wa Jengo la Trump mjini Moscow.

Trump Jr ameiambia Kamati ya Sheria ya Baraza la Seneti alipohojiwa mwaka 2017 kuwa alikuwa na "taarifa ya juu juu" kuhusu pendekezo la ujenzi huo.

Kamati ya Usalama ya Baraza la Seneti imeendelea kufanya uchunguzi juu ya Russia kuingilia kati uchaguzi na mafungamano ya Trump na Russia kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Huu ni wito wa kwanza unaojulikana wa mwanafamilia wa karibu na Rais Trump na ni ishara mpya kuwa jopo la Baraza la Seneti linaendelea na uchunguzi wake juu ya Russia hata baada ya Mwendesha Mashtaka Maalum Robert Mueller kutoa ripoti juu ya uchunguzi huo.

Haijafahamika mara moja iwapo mtoto wa Trump ataheshimu wito huo.

XS
SM
MD
LG