Mahakama hiyo imeamuru alipe faini na fidia ya jumla ya Shs milioni 273 ($119,000) baada ya kukiri makosa yaliyokuwa yanamkabili ya utakatishaji fedha na ukwepaji kodi. Wakati huohuo mahakama hiyo imemuondolea shitaka la kuongoza genge la uhalifu.
Mahakama imetoa uamuzi huo baada ya mazungumzo na makubaliano baina yake na Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP).
Kabendera amekiri shtaka la kukwepa kodi ya Shs milioni 173. Kwa mujibu mahakama ameahidi kulipa kiasi hicho kwa mafungu ndani ya kipindi cha miezi 6.
Pia kwa shtaka hilo, mahakama imeamuru alipe faini ya Shs 250,000 au kifungo cha miezi sita jela.
Kabendera amekiri pia shtaka la utakatishaji fedha na mahakama imeelezwa kuwa mwandishi huyo maarufu wa habari za kiuchunguzi, tayari ameshalipa kiasi cha Shs milioni 100 kama faini ya shtaka.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Tanzania