Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:29

Japan kuondoa hali ya dharura mjini Tokyo


Waziri Mkuu akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari. Raia wa Japan akimsikiliza kupitia luninga Jumatatu, Mei 25, 2020,
Waziri Mkuu akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari. Raia wa Japan akimsikiliza kupitia luninga Jumatatu, Mei 25, 2020,

Japan imepanga kuondoa hali ya dharura mjini Tokyo na wilaya nne jirani zilizokuwa katika hali hiyo mwezi uliopita katika kilele cha mlipuko wa virusi vya corona.

Waziri wa Uchumi Yasutoshi Nishimura amesema jopo maalum la virusi vya corona limeidhinisha mpango wa kuondoa amri hiyo kwa mji mkuu huo wa Japan na maeneo yanayo yazunguka baada ya idadi ya maambukizi mapya yalikuwa yameanza kupungua.

Waziri Mkuu Shinzo Abe atatangaza rasmi kuondolewa kwa hali hiyo ya dharura Jumatatu.

Waziri Mkuu awali alitangaza siku 30 za hali ya dharura Aprili 7 katika mji wa Tokyo na majimbo sita mengine, ikiwemo mji wa kati wa bandari wa Osaka, wakati idadi ya maambukizi ya COVID-19 yakiendelea kuongezeka.

Abe aliendeleza hatua hiyo ya dharura nchi nzima siku chache tu kabla ya muda wa amri hiyo kumalizika, na pole pole akaanza kuiondoa kwa kadri ya hali ilivyoonekana kuwa shwari. Amri hiyo ilikuwa awali imepangwa kumalizika Mei 31.

Japan imeripoti zaidi ya maambukizi 16,000 yaliyothibitishwa ya COVID-19 na vifo zaidi ya 800, hali ambayo imepelekea mifumo yake ya afya kuelemewa.

Pia hali hiyo imesababisha uchumi wake kudorora na kuilazimisha kuahirisha michezo ya Olympiki ya kipindi cha joto kwa mwaka mmoja. Kura ya maoni juu ya kukubalika kwa Waziri Mkuu Abe zinaonyesha kushuka kwa sababu ya kuchelewa kwake kuchukua hatua dhidi ya janga hilo.

Kutangazwa kwa hali ya dharura kulikuwa na ukomo wa kutotangaza amri ya kisheria ya watu kutotoka nje taifa zima, kwa sababu ya katiba ya Japan ya kipindi baada ya vita vya pili vya dunia ambayo inaipa uzito mkubwa wa upendeleo wa uhuru wa kiraia.

XS
SM
MD
LG