Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:54

COVID-19 : Marekani bado yaongoza katika maambukizi


Watu wakingojea kujiandikisha kupata posho kutokana na kupoteza ajira kwa sababu ya janga la corona, huko Fort Smith, Jimbo la Arkansas, Marekani April 6, 2020. REUTERS/Nick OxfordArkansas.
Watu wakingojea kujiandikisha kupata posho kutokana na kupoteza ajira kwa sababu ya janga la corona, huko Fort Smith, Jimbo la Arkansas, Marekani April 6, 2020. REUTERS/Nick OxfordArkansas.

Idadi ya watu walioambukizwa kote duniani Alhamisi ilikuwa imezidi million 3.8 na vifo ni zaidi ya 260,000 na wagonjwa zaidi ya million 1.3 wamepona, kulingana na ripoti ya kitengo kinachofuatilia maambukizi ya COVID-19 duniani, WorldOMeter.

Marekani bado inaongoza kwa idadi kubwa ya maambukizi ambapo yamezidi milioni 1.26, huku vifo vikizidi 73,000 katika ripoti ya Jumatano.

Wakati huo huo, majimbo 43 ya Marekani kati ya majimbo 50 yamepanga kufungua baadhi ya shughuli mwishoni mwa wiki hii, katika hali ya kulegeza masharti magumu yaliochukuliwa ili kuzuia kusambaa kwa virus vya corona.

Pamoja na hilo, wataalumu wa afya wanasema majimbo mengi bado yanakabiliwa na idadi kubwa ya maambukizi.

Katika kanda ya Afrika Mashariki na nchi za maziwa makuu, Shirika la Fedha Kimataifa, IMF, Jumatano liliidhinisha mkopo usiokuwa na masharti mengi na wenye kiwango cha chini cha riba wa dola million 739 utakaoisaidia Kenya kukabiliana na athari za kiuchumi, kutokana na janga la corona.

Wizara ya fedha ya Kenya inakadiria kuwa uchumi wa taifa utashuka kati ya asilimia 2,5 hadi asilimia 1.8 mwaka huu, ukilinganisha na asilimia 5.4 mwaka uliopita wa 2019.

Hadi jana, Kenya imethibitishwa kuna watu 581 walioambukizwa na virusi vya corona.

IMF imetoa pia mkopo huo wa dharura kwa Uganda, nchi hiyo imepewa dola million 491 kwa kupunguza athari za janga la corona kwenye uchumi wa taifa. Uganda sasa ina visa 100 vya maambukizi ya corona baada ya visa viwili vipya kuripotiwa hapo jana. Watu hao wawili waliokutwa wameambukizwa na madereva wa lori kutoka Kenya.

Nchini Rwanda, idadi ya maambukizi imefikia 268 baada ya visa vipya 7 kuthibitishwa na wizara ya afya hapo jana. Wizara hiyo inasema wagonjwa 130 walipona.

Nacho kitengo cha kitaifa kinachofuatilia magonjwa ya kuambukiza, Rwanda Biomedical Center, kimesema wilaya 13 za Rwanda zilipata angalao mtu mmoja aliyeambukizwa, nazo wilaya 17 hazijaripoti maambukizo yoyote.

Katika nchi jirani ya DRC, idadi ya waloambukizwa imefikia 863 baada ya watu 66 wepya kuripotiwa jana. Watu 36 wamerafiki, nao wagonjwa 103 walipona, kulingana na taarifa ya kitengo cha kitaifa cha kupambana na covid 19.

Tanzania na Burundi hazijatoa taarifa yoyote mpya kuhusu maambukizi ya corona.

Katika bara la Ulaya, Spain, Italy, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Uholanzi na Sweden hazikuripoti mtu yeyote aliyeambukizwea katika saa 24 zilizopita.

Ubeljiji imethibitisha watu wepya 639 pamoja na vifo 76 mnamo saa 24 zilizopita. Russia imeripoti watu elfu 11 na 231 waloambukizwa na vifo 88.

Katika bara la Asia, China imeripoti watu 2 wapya katika saa 24 zilizopita, Japan haikuripoti mtu yeyote, nayo Korea Kusini imethibitisha watu wanne wengine na kifo kimoja.

Huko Amerika Kusini, Mexico imeripoti watu wengine 1 609 aloambukizwa pamoja na watu 197 kufariki mnamo saa 24 zilizopita.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Patrick Nduwimana, Washington, DC

XS
SM
MD
LG