Idadi hiyo ndio ya juu zaidi nchini humo kutangazwa kwa siku moja, tangu nchi hiyo ilipotangaza kisa cha kwanza cha maambukizi ya corona, mwezi Machi.
Watu 69 wamethibitishwa kuambukizwa katika mji mkuu wa Kinshasa na 23 katika mkoa wa kati ya Congo.
Watu wengine 212 wanachunguzwa kubaini iwapo wameambukizwa virusi hivyo.
Watu 104 wakiwemo wafungwa na walinzi wa magereza, wameambukizwa corona katika gereza la Ndolo, mjini Kinshasa.
Waziri wa Afya ya Umma Eteni Longondo, amesema hali imedhibitiwa, licha ya ongezeko la idadi ya watu wanaoambukizwa. Amesema kwamba serikali inafikiria kufungua shule.
Kufikia sasa, watu 705 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya corona na 34 kuaga dunia, nchini DRC.