Kamerhe anashtakiwa pamoja na mfanyabiashara mwenye asili ya Lebanon pamoja na mshauri mwengine wa rais kuhusiana na mradi wa sku 100 wa Rais Felix Tshisekedi.
Kulingana na wakili wa Vital Kamerhe ni kwamba mahakama ilipokea rasmi mashtaka ya uchunguzi kutoka kwa waendesha mashtaka siku ya Jumatatu na ombi lao la kutaka kuachiliwa mteja wao kwa dhamani.
Khamere ambaye ni Mkuu wa utawala wa Rais Felix Tshisekedi ambaye yuko jela kwa siku 16 sasa, anakanusha tuhuma hizo kuhusiana na ubadhirifu wa mali kuhusiana na mradi wa ujenzi wa miundo mbinu na makazi ya watu wa mapato ya chini ulioahidiwa na Rais Tshisekedi kuanza katika siku 100 za mwanzo wa utawala wake.
Watu wengine wawili wanaoshtakiwa ni Jammal Sammih mfanyabiashara mwenye asili ya Lebanon aliyepewa kandarasi ya kujenga nyumba za watu wa tabaka la chini.
Kesi ya pili inahusu kandarasi iliyopewa kampuni ya Trade Plus kuagizia dawa ingawa hiyo sio fani yake. Jumatano Waziri wa Elimu ya Juu Thomas Luhaka anasikilizwa na mahakama ya kukata rufaa kuhusiana na mradi huo wa siku 100 kwa vile alikuwa waziri wa miundo mbinu , ukarabati na kazi za umaa wakati wa kuzinduliwa mradi huo.
Imetayarishwa na Mwandishi wetu Abdushakur Aboud, Washington, DC.