Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:08

Hatma ya mgogoro wa Rwanda, Uganda uko mikononi mwa Kagame, Museveni - Wachambuzi


Rais Paul Kagame na Rais Museveni
Rais Paul Kagame na Rais Museveni

Pamoja na kuwa wanashirikiana katika mipaka yao na kuwepo kwao katika wigo la kiuchumi la pamoja, nchi za Afrika Mashariki zinakuwa na hisia kali baina yao zinazotokana na tofauti zao za kiuchumi na kisiasa.

Kwa mujibu wa gazeti la The East African, nakala ya Jumapili, aghlabu, mivutano hiyo ni mfukuto wa chini kwa chini au baadhi ya wakati inageuka kuwa matamko hasi yanayofanywa hadharani, na hakuna yeyote anaetabiri mapambano ya kutumia silaha baina yao.

Juhudi za kurejesha mahusiano kati ya Rwanda na Uganda mpaka sasa hazijazaa matunda wakati mazungumzo ya kidiplomasia yaliyomalizika wiki mbili zilizopita yaligonga ukuta, pande zote mbili zikimshutumu mwenzake kutokana na kukwama kwa mazungumzo hayo.

Lakini wachambuzi wa kisiasa wanasema matumaini yote yanategemea marais Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda ambao wajumbe wao walioko katika mazungumzo yanayosuasua huko Kampala wamesema tayari wameshauriana na wakuu wa nchi zao husika.

Lakini hivi karibuni, na hasa mwaka 2019, migogoro hii imeongezeka “kufikia vita baridi” kati ya Uganda na Rwanda na Rwanda na Burundi, na huku Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zikiwa zinaendelea kuimarisha maelewano yao.

Mwaka 2019 migogoro ya kidiplomasia na usalama biana ya Rwanda na Uganda iliongezeka na kufikia viwango vilivyokuwa havijawahi kushuhudiwa. Kwa mara ya kwanza, nchi hiyo ilijitokeza hadharani na kuishutumu vikali Uganda kuwa inawasaidia waasi ambao wanataka kuleta mabadiliko ya kiutawala Kigali.

Kadhalika, Rwanda nayo iliishutumu Uganda kwa kuhujumu miradi ya miundombinu ya pamoja, biashara na vitendo vya kuwatesa raia wa Rwanda ambao wanatembelea Uganda. Kigali ilifunga mipaka yake na Uganda na kuwaamrisha raia wake kutotembelea Uganda.

Hata hivyo Uganda imekanusha tuhuma zote hizo zilizoelezewa na Rwanda.

Kufungwa kwa mpaka kulikotekelezwa Machi 2019, kuliyumbisha maisha ya jamii na uchumi siyo tu ya watu wanaoishi kuzunguka maeno ya mpaka huo lakini pia usafiri na biashara ya kitaifa baina ya nchi hizo mbili.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, tangu mwaka 1990 vita vya kutumia waasi ndani ya DRC, wakati nchi ya Uganda na Rwanda ziliendelea kuvisaidia vikundi mbalimbali, mahusiano ya kidiplomasia na kiusalama kati ya nchi hizi mbili yaliendelea kuzorota na kufikia kuwa dhaifu kabisa mwaka 2019.

XS
SM
MD
LG