Wanafamilia wengine walieleza matumaini kuwa hukumu hiyo itakuwa ni kiini cha mabadiliko.
Mmoja wa kaka zake Floyd, Rodney Floyd, ameiita hukumu hiyo ni “kumpiga kofi mhalifu kwenye kiganja.”
“Sisi tunaumia kwa kifungo cha maisha kwa kumpoteza ndugu yetu maishani, na hilo linaniumiza hadi mwisho wangu duniani,” amesema
Ndugu mwengine, Terrence Floyd, amesema “alikuwa na mashaka juu ya hukumu hiyo” mpaka alipoota na kumuona baba yake.
“Najua baba yangu alikuwa akisema, ‘Uko vizuri, yeye yuko vizuri, endelea kufanya unacho kifanya. Kwa ajili yangu na ndugu yako, kwa ajili ya jina lako,”’ alisema. “Tuko imara kwa ajili ya Floyd, na tutaendelea kuwa imara.”
Bridgett Floyd, dada ya George Floyd na muasisi wa Taasisi ya Kumbukumbu ya George Floyd, amesema hukumu hiyo “inaonyesha hatua dhidi ya ukatili unaofanywa na polisi hatimaye unachukuliwa hatua ipasavyo.”