Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:13

Wizara ya Sheria ya Marekani imefungua uchunguzi katika idara ya polisi ya Minneapolis


Mwanasheria mkuu Merrick Garland akizungumza juu ya matokeo ya kesi dhidi ya afisa wa polisi wa zamani Derek Chauvin katika wizara ya sheria mjini Washington, D.C., U.S. April 21, 2021. (Andrew Harnik/Pool vi
Mwanasheria mkuu Merrick Garland akizungumza juu ya matokeo ya kesi dhidi ya afisa wa polisi wa zamani Derek Chauvin katika wizara ya sheria mjini Washington, D.C., U.S. April 21, 2021. (Andrew Harnik/Pool vi

Wizara ya Sheria ya Marekani imefungua uchunguzi wa haki za kiraia katika idara ya polisi iliyo matatani katika mji wa Minneapolis Minnesotta.

Mwanasheria Mkuu wa Marekani Merrick Garland alitangaza siku ya Jumatano, siku moja baada ya baraza la mahakama kumtia hatiani afisa wa polisi wa zamani wa Minneapolis Derek Chauvin katika mauaji ya George Floyd.

Afisa huyo wa zamani wa polisi mzungu alihukumiwa kwa makosa matatu katika mauaji ya George Floyd, Mmarekani mweusi aliyefariki dunia baada ya kubanwa kwenye shingo na goti la Chauvin kwa zaidi ya dakika tisa.

Uchunguzi huo utaangalia ikiwa Idara ya Polisi ya Minneapolis imehusika katika mfumo au kazi ya kipolisi kinyume cha katiba, Garland alisema katika wizara ya Sheria.

Pia itaangalia matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji na ikiwa jinsi wanavyowafanyia watu wenye ulemavu wa akili wanakiuka sheria za serikali kuu.

XS
SM
MD
LG