Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 11:57

Wamarekani washukuru katika kipindi cha sikukuu, lakini ... - Tafiti


Shamra shamra za sikukuu ya Krismas katika Kanisa la Nativity, lililojengwa katika eneo linalosadikiwa kuwa Yesu Kristo alizaliwa, wakati wa kilele cha Krismas, huko Bethlehem, 2017.
Shamra shamra za sikukuu ya Krismas katika Kanisa la Nativity, lililojengwa katika eneo linalosadikiwa kuwa Yesu Kristo alizaliwa, wakati wa kilele cha Krismas, huko Bethlehem, 2017.

Wade Holcomb ana mengi ya kushukuru kwa mwaka 2019. Likiwemo la kumaliza masomo chuo kikuu na kupata kazi. Pia ana mtoto mremo wa kike wa miezi minne -- ambaye atasheherekea sikukuu ya Krismas.

"Ni kitu tofauti, kupata mtoto. Ni kitu cha kushukuru kwacho na kina nifanya niwe mwenye furaha zaidi katika ulimwengu huu," amesema Holcomb, 22, anayeishi Swainsboro, Georgia. Hasa mtoto wangu ni kitu bora zaidi kuliko chochote nilichopata."

Holcomb ni kati ya Wamarekani 7 kati ya 10 ambao wanasema "shukurani" inawaelezea vizuri zaidi au vizuri sana katika sikukuu hizi, kwa mujibu wa maoni mapya yaliyokusanywa na chombo cha habari cha The Associated Press -Kituo cha NORC kinachofanya tafiti za Masuala ya Umma. Kwa makadirio watu wawili wengine kati ya 10 walisema shukrani inawaelezea kwa wastani wa kuwa wako vizuri.

Wakati hisia chanya ndiyo zinazoongoza, hisia za sikukuu na shukrani zimeambatana na shinikizo la maisha na majonzi kwa Wamarekani wengi. Karibu watu watatu kati ya kumi wanasema "shinikizo la maisha" linaeleza hali zao za kuwa wako vizuri au vizuri sana katika Mwezi wa Disemba, na takriban wengine 4 kati ya 10 wanasema inawaelezea hali zao kuwa nzuri kwa wastani.

Watu wawili kati ya 10 wanahisi wako wapweke au wanamajonzi wakati wa sikukuu, na wengine wawili kati ya kumi wakisema wanajihisi kwa wastani wapweke au wanamajonzi.

Afya na familia

Kwa wale wanaohisi wanashukuru, hali ya kuwa wana afya nzuri na kuwa wamezungukwa na familia ndio lililoko katika fikra zao. Wakati Holcomb anashukuru kwa maisha mapya katika familia yake, Steven Tutunjian mwenye umri wa miaka 76 wa San Diego anashukuru kuwa bado anaishi.

Tutunjian alilazwa hospitali mara tatu katika miezi ya karibuni kutokana na matatizo ya kupumua, ikiwemo kupelekwa hospitali katika hali ya dharura na kuwekwa katika uangalizi maalum katika wiki za karibuni. Huko ndiko alipokuwa wakati anahojiwa na AP-NORC.

"Kwa sababu ya upendo wa Mungu, ndiyo maana niko bado hai," amesema. "Ile tu kutambua kuwa bado unaishi, una afya na kupata nafuu kama nilivyo mie -- huna la kufanya ila kushukuru."

Mila

Maoni haya yalibaini kuwa takriban Wamarekani 6 kati ya Kumi wanasema wanasubiri kushiriki katika mila za kifamilia mwaka 2019, wakati mtu mmoja kati ya 10 wanasema wanasubiri kushiriki lakini kwa wasiwasi mkubwa.

XS
SM
MD
LG