Wamarekani wapo katika siku nyingine inayojulikana kama Black Friday, ambayo huanza saa chache baada ya kumaliza mlo unaoambatana na milo midogo midogo mingi katika sherehe za sikukuu ya shukrani, Thanksgiving.
Black Friday ni muda maalumu ambapo maduka hufunguliwa wakati wa jioni na bidhaa huuzwa kwa bei ya chini mno kuliko mteja anavyotarajia. Wamarekani wamekuwa wakiitumia siku hii kununua bidhaa ambazo zinaashiria kuanza kwa maandalizi ya zawadi za Krismas na kufunga mwaka.
Watu wanasubiri kwa hamu kuona maduka makubwa kama vile Macy’s, JCPenney, Best Buy, Walmart na Target yatakuwa na bidhaa gani kwenye siku ya Black Friday, na kwa bei gani kulinganisha na siku za kawaida.
Hali kadhalika maduka mengi ya kibiashara yanayopatikana katika eneo moja maalumu yaani Mall yalifunguliwa mapema mno au alfajiri ya Ijumaa.
Chama cha biashara Marekani, The National Retail Federation kinatabiri kwamba mauzo ya kipindi cha sikukuu yataongezeka kwa asilimia 3.6 zaidi ya mwaka uliopita wa 2015 kufikia dola 655.8 bilioni