Mchambuzi wa ngazi ya juu wa kikundi kinachoshugulikia migogoro ya kimataifa Casie Copeland amesema kulikuwa na wasiwasi kabla ya kufikiwa makubaliano hayo iwapo mkataba huo utasainiwa, baada ya pande zote mbili, serikali na kikundi kikubwa cha upinzani kuibua changamoto muhimu katika rasimu ya mkataba huo.
“Serikali imeibua masuala kadhaa na ukweli kuwa mkataba usinge waruhusu kupata silaha tena kwa ajili ya madhumuni yoyote mengine, kama vile kwa ajili ya kutekeleza sheria na utulivu, na upinzani unafikiria kuwa muundo wa wasimamizi wa hatua ya kusitisha mapigano na waangalizi wa amani unatakiwa upitiwe upya kutokana na kubadilika kwa mazingira.”
Hatimaye, amesema kuwa mkataba umezingatia vifungu ambavyo vinaziridhisha pande zote mbili.