Msemaji wa Bunge la China amesema kwamba msimamo wa kisheria wa China unabaki ule ule wa kutambua kwamba ndoa ni kati ya mwanamume na mwanamke.
Mwezi Mei 2019 Taiwan ilikuwa taifa la kwanza la Asia kuidhinisha ndoa ya watu wa jinsia moja baada ya mjadala wa miaka mingi juu ya usawa wa ndoa.
Wachambuzi wanasema kuna jamii kubwa ya mashoga katika miji mikubwa ya China.
katika miezi ya hivi karibuni jamii hiyo imekuwa ikilengwa kwa kuhesabiwa na kuzusha hofu huenda wachina wakaanza kutowastahmilia.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.