Kusitishwa kwa shughuli za kiwanja hicho kunatokana na shinikizo la waandamanaji ambao ni wanaharakati wa mji huo ambao wamevamia uwanja huo na kusababisha shughuli zote kusimama.
Polisi wa Hong Kong wamewaambia waandishi habari kwamba karibu wanaharakati elfu 5 waliwasili na kukusanyika kwenye ukumbi wa kuondoka wasafiri kwa siku ya nne Jumatatu.
Wakati huo huo Darzeni ya waandamanaji wamejeruhiwa Jumatatu katika mitaa mingi ya Jimbo la Hong Kong katika mapambano na polisi wa kuzuia ghasia.
Waandamanaji wenye hasira wamezuia barabara na kukaidi amri ya polisi ambao wametumia gesi ya kutoa machozi na risasi za plastiki kuwatawanya waandamanaji.
Serikali ya jimbo la Hong Kong iliyo chini ya mamlaka ya China inasema watu 54 wamejeruhiwa katika ghasia hizo. Viongozi wa china wametaja maandamano ya Jumatatu kama vitendo vya ugaidi.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.