Baadhi ya wachambuzi wanasema uwepo wa wanajeshi hao ni ishara ya ujumbe kutoka Beijing kwamba ipo tayari kutumia nguvu kuvunja maandamano ya kudai mabadiliko ya demokrasia, Hong Kong.
Wakaazi wa Hong Kong wamekuwa wakiandamana wakidai kunyimwa uhuru wa kufanya mambo yao na Hong Kong kuingiliwa na China bara katika masuala ya jimbo hilo.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema makubaliano ya biashara kati ya Marekani na China huenda yakachelewa hadi pale hali ya utulivu itakapopatikana Hong Kong.
Trump alipendekeza kuwa mpatanishi kati ya serikali ya China na waandamanaji, ili kumaliza mgogoro wa Hong Kong.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.