Ameeleza kuwa kampuni yake haitapata shida yoyote kwa kukosa kutumia vifaa maalum vya kunasa mawasiliano vinavyotengenezwa Marekani.
Idara ya viwanda na usalama katika Wizara ya Biashara ya Marekani, imeiweka kampuni ya Huawei na washirika wake katika orodha ya makundi ya kampuni zinazokatazwa kuuza au kuhamisha teknolojia za Marekani.
Katika mahojiano na shirika la habari la Nikkei, Japan, Ren amekosoa utawala wa Rais Donald Trump kwa kuiorodesha Huawei na washirika wake kwa madai ya kuwa kampuni hiyo ni tishio kwa uslama wa taifa, akiongezea kwamba kampuni hiyo haijafanya kitu chochote kibaya.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.