Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:17

CCM yazindua rasmi kampeni kuelekea uchaguzi mkuu 2020


Picha ya Kumbukumbu : Rais Pombe Magufuli Mgombea kiti cha urais wa CCM akiwa jukwani na wanamuziki.
Picha ya Kumbukumbu : Rais Pombe Magufuli Mgombea kiti cha urais wa CCM akiwa jukwani na wanamuziki.

Chama cha Mapinduzi nchini Tanzania leo Jumamosi kimezindua rasmi kampeni zake kuelekea uchaguzi mkuu 2020, katika uwanja wa Jamhuri Dodoma, ambapo wasanii zaidi ya 100 wanashiriki kutumbuiza katika uzinduzi huo.

Rais John Pombe Magufuli ambae anaomba ridhaa ya kuongoza muhula wa pili kwa tiketi ya chama tawala cha CCM, ajenda yake inatarajiwa kujikita katika kueleza mafanikio ya chama chake kati ya mambo mengine kama vile kukabiliana na ufisadi na kurejesha nidhamu serikalini.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Tanzania mamia ya wananchi wamefurika uwanjani hapo kushuhudia uzinduzi huo.

Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameongoza ufunguzi huo.

Wakati huohuo viongozi mbalimbali wa serikali na CCM wakiwemo marais wastaafu wamehudhuria ufunguzi huo.

Wakati kampeni hizi zikiendelea upinzani katika ajenda yao wamejikita kuelezea kuminywa kwa haki za binadamu, uhuru wa kujieleza na haki za kiraia.

CCM ni ya pili kuzindua kampeni baada ya chama kikuu cha upinzani Chadema kufanya uzinduzi wake Ijumaa mjini Dar es Salaam.

XS
SM
MD
LG