Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 20:04

Burundi: Watoto 4 wafariki baada ya kanisa kuporomoka kufuatia mvua kubwa


Mafuriko
Mafuriko

Mvua kubwa iliyonyesha kusini mwa Burundi imesababisha vifo vya watoto wanne baada ya kanisa walimokuwa kuporomoka huku watu  wengine 15 wakijeruhiwa siku ya Jumapili, kulingana na afisa wa eneo hilo na vyombo vya habari vya serikali.

Mvua kubwa ikiandamana na upepo mkali ilianza kunyesha Kiyange mwendo wa saa moja asubuhi, afisa wa serikali ya mtaa Esperance Inarukundo aliliambia shirika la habari la AFP.

Hali mbaya ya hewa "ilisababisha uharibifu mkubwa, ikiwa ni pamoja na kuporomoka kwa kanisa la kipentekoste la Kiyange," ambapo watoto walikuwa wakihudhuria madarasa ya elimu ya dini, Inarukundo alisema.

"Tunaendelea na upekuzi kwenye vifusi na tayari tumegundua miili ya watoto wanne waliokufa na majeruhi 15 kanisani," alisema na kuongeza kuwa wakaazi wa eneo hilo, Shirika la Msalaba Mwekundu la Burundi na idara ya ulinzi wa raia walikuwa wakisaidia shughuli ya uokoaji.

Shirika la Habari la Burundi linalomilikiwa na serikali lilithibitisha idadi ya waliofariki kwenye mtandao wa X, uliojulikana zamani kamaTwitter, likisema kuwa "ukuta wa kanisa uliangukia watoto hao.

Burundi ambayo ni nyumbani kwa watu milioni 12, ni moja ya nchi maskini zaidi duniani.

Forum

XS
SM
MD
LG