Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 01:20

Mvua kubwa zimeathiri juhudi za kuwatafuta wanajeshi 23 wa India waliotoweka kufuatia mafuriko


Mafuriko katika Jimbo la Sikkim, India.
Mafuriko katika Jimbo la Sikkim, India.

Mvua kubwa imeathiri juhudi za kuwatafuta wanajeshi 23 wa India walioripotiwa kutoweka Jumatano baada ya kutokea mafuriko ya ghafla katika jimbo la Sikkim, kaskazini mwa nchi hiyo.

Maafisa katika wizara ya ulinzi wamesema kwamba usafiri kuelekea mji mkuu wa jimbo hilo wa Gangtok umetatizika baada ya barabara kufunikwa na mafuriko.

Msemaji wa wizara ya ulinzi amesema kwamba maafisa 23 hawajulikani walipo, na baadhi ya magari yamesombwa na mafuriko, akiongezea kwamba juhudi za uokoaji zinaendelea.

Idara ya hali ya hewa nchini India imeonya kwamba kuna uwezekano wa kutokea maporomoko ya ardhi na kuvurugika kwa safari za ndege, mvua kubwa ikiendelea kunyesha katika baadhi ya sehemu za Sikkim.

Barabara kuu inayounganisha Sikkim na jimbo la magharibi la Bengal, imafunikwa na maji na hakuna usafiri kuelekea Gangtok.

Baadhi ya kambi za jeshi katika sehemu hiyo ya bonge zimeathiriwa na mafuriko hayo.

Forum

XS
SM
MD
LG