Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 06:13

Kauli za chuki dhidi ya Waislam India zimeongezeka kipindi cha uchaguzi - ripoti


FILE - Waziri Mkuu Narendra Modi akizungumza baada ya uzinduzi wa jengo jipya la bunge, New Delhi, Mei 28, 2023.
FILE - Waziri Mkuu Narendra Modi akizungumza baada ya uzinduzi wa jengo jipya la bunge, New Delhi, Mei 28, 2023.

Matukio haya yamejitokeza zaidi katika majimbo yanayo jiandaa kwa uchaguzi, kulingana na ripoti ya taasisi ya Hindutva Watch, kikundi chenye makazi yake Washington kinachofuatilia mashambulizi dhidi ya walio wachache.

Kulikuwa na matukio 255 yaliyorekodiwa ya mikusanyiko inayotoa kauli za chuki kuwalenga Waislam katika nusu ya kwanza ya m waka 2023, ripoti hiyo imegundua. Hakuna takwimu za kulinganisha hali hiyo na miaka iliyopita.

Ripoti ilitumia ufafanuzi wa Umoja wa Mataifa wa kauli za chuki kuwa “ ni aina yoyote ya mawasiliano… yanayotumia lugha ya ubaguzi au unyanyapaa dhidi ya mtu au kikundi kwa misingi kama vile wasifu wa dini, ukabila, utaifa, nasaba, rangi, asili, jinsia, au utambulisho mwingine.”

Takriban asilimia 70 ya matukio hayo yamefanyika katika majimbo yanayaotarajiwa kuitisha uchaguzi mwaka 2023 na 2024, kulingana na ripoti.

Maharashtra, Karnataka, Madhya Pradesh, Rajasthan, na Gujarat zimeshuhudia idadi ya juu zaidi ya mikusanyiko inayotoa kauli za chuki, huku Maharashtra ikiwa na asilimia 29 ya matukio hayo, ripoti hiyo imebaini.

Matukio mengi zaidi ya kauli za chuki yamekuwa yakitaja nadharia za hujuma na wito wa ghasia na migomo ya uchumi wa kijamii dhidi ya Waislam.

Kiasi cha asilimia 80 ya matukio hayo yalitokea katika maeneo yanayoongozwa na Chama cha Hindu Nationalist Bharatiya Janata Party (BJP) cha Waziri Mkuu Narendra Modi, ambacho kinatarajiwa kwa kiasi kikubwa kushinda uchaguzi mkuu mwaka 2024.

Hindutva Watch ilisema iligundua harakati katika mitandao ya vikundi vya wazalendo wa Kihindu, imethibitisha kanda za video za kauli za chuki zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii na kukusanya takwimu ya matukio maalum yaliyoripotiwa na vyombo vya habari.

Serikali ya Modi inakanusha uwepo wa ukandamizaji wa makundi ya walio wachache. Ubalozi wa India mjini Washington haukujibu ombi la kutoa maoni yao.

Vikundi vya kutetea haki vinadai kutendewa vibaya kwa Waislam chini ya Modi, ambaye amekuwa waziri mkuu mwaka 2014.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG