Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:21

Viongozi wa mataifa ya G20 mjini New Delhi watofautiana kuhusu vita vya Ukraine kabla ya mkutano kufunguliwa


Wajumbe wanawasili kwenye mkutano wa kilele wa mataifa yaliyoendelea kiviwanda G20, mjini New Delhi India.
Wajumbe wanawasili kwenye mkutano wa kilele wa mataifa yaliyoendelea kiviwanda G20, mjini New Delhi India.

Rasimu hiyo ya kurasa 38 ilisambazwa miongoni mwa wanachama iliacha wazi aya kuhusu “hali ya kisiasa ya kikanda” wakati ilikubaliwa kuhusu aya nyingine 75 ambazo zilijumuisha mabadiliko ya hali ya hewa, sarafu ya crypto na mageuzi katika mabenki mbali mbali ya maendeleo.

Waandaaji wa mkutano G20 wamekuwa wakijitahidi kwa siku kadhaa kukubaliana juu ya lugha kwasababu ya tofauti kuhusu wa vita, wakitumaini kuipata Russia katika kuandaa waraka wa pamoja.

Mjumbe wa India katika G20, Amitabh Kant, alisema awali katika siku kuwa “Azimio la Viongozi la New Delhi linakaribia kuwa tayari. Hili tangazo litalipendekeza kwa viongozi.”

Amitabh Kant, msimamizi mkuu wa mkutano wa kilele wa G20, akizungumza na waandishi habari siku ya Ijuma.
Amitabh Kant, msimamizi mkuu wa mkutano wa kilele wa G20, akizungumza na waandishi habari siku ya Ijuma.

Chanzo kimoja kimeiambia Reuters kuwa tangazo la pamoja huenda likatolewa kwa makubaliano ya wote au la. Huenda likawa na aya za maoni ya nchi tofauti. Au huenda likarekodi makubaliano na kutokukubaliana katika aya moja.

Kwa mujibu wa chanzo kingine cha juu katika moja ya nchi wanachama wa G20, aya kuhusu vita vya Ukraine limekubaliwa nan chi za Magharibi na lilipelekwa kwa Russia kwa maoni yake.

Afisa huyo alisema Russia ilikuwa na njia mbadala kukubali maoni ya nchi za Magharibi na kutoa maoni yake kama sehemu ya taarifa. Kutofikiwa kwa makubaliano, India itatakiwa kutoa taarifa ya mkutano kama mwenyekiti, ambayo itamaanisha kwamba G20 kwa mara ya kwanza katika miaka 20 haitakuwa na tangazo.

Mkutano wa siku mbili wa viongozi unaanza Jumamosi mjini New Delhi ulitarajiwa kutawaliwa na Magharibi na washirika wake. Rais wa China Xi Jinping hatakwenda katika mkutano na kumpeleka Waziri Mkuu Li Qiang badala yake, wakati Vladimir Putin wa Russia pia hatakuwepo kwenye mkutano.

Rais Joe Biden wa Marekani atizama kundi la wachezaji ngoma za asili alipowasili kwenye uwanja wa dege wa Indira Gandhi.
Rais Joe Biden wa Marekani atizama kundi la wachezaji ngoma za asili alipowasili kwenye uwanja wa dege wa Indira Gandhi.

Rais wa Marekani Joe Biden, Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak, Mohamed Bin Salman wa Saudi Arabi na Fumio Kishida wa Japan, ni miongoni mwa wale ambao watahudhuria.

Msimamo mkali juu ya vita umezuia makubaliano kwa hata taarifa moja ya pamoka katika mikutano ya ngazi ya mawaziri wakati wa urais wa India wa G20 hadi hivi sasa mwaka huu, na kuwaacha viongozi kutafuta njia ya kuzunguka hilo kama itawezekana.

China ilisema Ijumaa iko tayari kufanya kazi na pande zote ili kuweze kupatikana matokeo chanya katika mkutano huo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Mao Ning alitoa matamshi baada ya ripoti za vyombo vya habari kusema Sunak ameilaumu China kwa kuchelewesha makubaliano kuhusu masuala mbali mbali, ikiwa ni pamoja na Ukraine. Huko New Delhi, Sunak alisema hiyo haikuwa sehemu kuiambia India kuhusu msimamo wa kuchukua juu ya vita nchini Ukraine.

India imekwepa kuilaumu Moscowa kwa vita na imetaka lipatikane suluhisho kupitia majadiliano na diplomasia. Gazeti la Financial Times siku ya Alhamisi kwamba Sunak atamsihi mwenzake wa India “kuieleza” kuhusu uvamizi wa Russia wa Februari 2022.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza na waandishi habari kabla ya kufunguliwa mkutano wa G20 mjini New Delhi.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza na waandishi habari kabla ya kufunguliwa mkutano wa G20 mjini New Delhi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Gueterres alisema viongozi wa G20 wana mamlaka ya kuushughulikia mzozo wa hali ya hewa ambao “unaoelekea kwenda bila ya udhibiti” na kuwasihi kurekebisha kanuni za ulimwengu za kifedha ambazo amezielezea kuwa zimepitwa na wakati na si za haki.

“Mzozo wa hali ya hewa unazidi kuwa mbaya – lakini majibu ya pamoja hayana utashi, hadhi, na uharaka,” Guterress alisema katika hotuba yake.

Forum

XS
SM
MD
LG