Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 02:04

Burundi: Wawili wauawa baada ya gari lao kuvamiwa

Maafisa wa polisi wa Burundi wakipiga doria.
Maafisa wa polisi wa Burundi wakipiga doria.

Watu wawili waliuawa na mwingine kujeruhiwa wakati gari lao lilipovamiwa na watu wenye silaha magharibi mwa Burundi karibu na mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wakazi walisema Jumapili.

Watu wawili waliuawa na mwingine kujeruhiwa wakati gari lao lilipovamiwa na watu wenye silaha magharibi mwa Burundi karibu na mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wakazi walisema Jumapili.

Shambulio hilo lilitokea katika barabara ya kutokamkoa wa Bubanza kuelekea mji mkuu wa kibiashara wa Burundi, Bujumbura, Wakazi walisema.

Watu watatu wameliambia shirika la habari la Reuters kuwa walisikia milio ya risasi na milipuko ya guruneti kutoka eneo la shambulio hilo.

Walisema wanashuku shambulizi hilo lililotokea umbali wa kilomita 5, kutoka mpakani, lilitekelezwa na Red-Tabara, kundi la waasi ambalo limekuwa likipambana na serikali ya Burundi kwa miaka kadhaa kutoka katika kambi za mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Walisema washambuliaji walirejea katika msitu wa Rukoko, ambapo wangeweza kuvuka kurudi kwenye ngome zao.

Kundi hilo hapo awali limekuwa likilaumiwa na serikali ya Burundi kwa kufanya mashambulizi kadhaa ya kuvizia, yakilenga raia na wanajeshi tangu mwaka wa 2015.

Polisi hawakupatikana kuzungumzia suala hilo Jumapili, kwa mujibu wa shirika la hanbari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG