Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:06

Burundi yashutumiwa kwa kuondoka kwa kikao cha kutathmini rekodi yake ya haki za binadamu


Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye.
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye.

Mashirika ya kutetea haki za kiraia siku ya Jumanne yalilaani uamuzi wa Burundi wa kuondoka katika kikao cha kamati ya  kutathmini  rekodi yake ya haki za binadamu na kuelezea wasiwasi wao kuhusu hali ya kupungua kwa ushirikiano wa baadhi ya nchi na mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Hali ya nchi kufuata mikataba ya haki za binadamu iliyo na uzito wa kisheria ambayo inahakikisha uhuru muhimu hufanyiwa tathmin ya mara kwa mara na Umoja wa Mataifa.

Lakini katika hali isiyo ya kawaida, wajumbe 15 wa Burundi walitoka nje ya kikao cha Kamati ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu mjini Geneva kwa sababu ya kile ilichokiita “kuwepo kwa wahalifu wanaojifanya wanachama wa mashirika ya kiraia.”

Tukio hilo linafuatia kukataa kwa Nicaragua kushiriki katika mchakato wa tathmini ya mateso na kutokuwepo kwa Russia katika tathmini mbili za mwaka jana, jambao ambaloi mkuu wa shirika la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa Volker Turk, alielezea mwezi Juni kama "ukosefu mkubwa wa ushirikiano" na mfumo wa haki za binadamu.

"Kuna mazoea na hili linazidi kuwa tatizo. Hapo awali, mataifa yalikuwa na hakika kwamba hili lilikuwa muhimu, lakini kumekuwa na upungufu wa ushirikiano katika siku za hivi karibuni kuhusu mkataba wa Umoja wa Mataifa," Patrick Mutzenberg, Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Kiraia na Kisiasa, aliliiambia shirika la habari la Reuters. .

Mwanasheria wa Burundi na mtetezi wa haki za binadamu Armel Niyo-ngere alisema maafisa wa serikali walijiondoa kwenye Kamati ya Haki za Kibinadamu dakika chache baada ya kikao kuanza juu ya uwepo wake katika mkutano huo. Niyo-ngere anaishi uhamishoni baada ya kushiriki katika maandamano ya 2015.

Forum

XS
SM
MD
LG