Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 10:29

Kikosi cha Afrika, Somalia chapanga kuondoka


Kikosi cha Umoja wa Afrika katika taifa la  Somalia lililokumbwa na migogoro kimesema kimekamilisha awamu ya kwanza ya kupunguza wanajeshi kwa lengo la kuweka suala la usalama mikononi mwa jeshi la taifa na polisi.

Kikosi cha kulinda amani cha Afrika nchini Somalia (ATMIS) kilisema katika taarifa yake ya Ijumaa kwamba jumla ya kambi saba zimekabidhiwa kwa vikosi vya usalama vya Somalia, na hivyo kuwezesha kupunguzwa kwa wanajeshi 2,000 kufikia tarehe ya mwisho ya Juni 30.

Afisa mkuu wa vifaa wa ATMIS, Bosco Sibondavyi alielezea makabidhiano hayo kama hatua muhimu katika utekelezaji wa mpango wa mpito wa Somalia na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu uhamishaji wa jukumu la usalama.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumanne liliidhinisha uwepo wa kikosi cha AU kwa miezi sita, ambapo muda wake unamalizika mwishoni mwa Septemba na kuondoa wanajeshi wengine 3,000.

Kikosi cha ATMIS kilikuwa kimejumuisha zaidi ya askari 19,000 na maafisa wa polisi kutoka mataifa kadhaa ya Afrika yakiwemo Burundi, Ethiopia, Kenya na Uganda, lakini italazimika kupunguzwa na kutokuwepo kabisa mwishoni mwa 2024.

Forum

XS
SM
MD
LG