Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 20:35

Tume ya uchaguzi Liberia yatangaza matokeo ya awali


Rais wa Liberia aliyepo madarakani George Weah na mpinzani wake mkuu Joseph Boakai. Picha na JOEL SAGET na Brendan SMIALOWSKI / AFP.
Rais wa Liberia aliyepo madarakani George Weah na mpinzani wake mkuu Joseph Boakai. Picha na JOEL SAGET na Brendan SMIALOWSKI / AFP.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Liberia, NEC, Jumatano ilitangaza kundi la kwanza la matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais na bunge uliofanyika Jumanne. Wakati takwimu zinawakilisha sehemu ndogo tu ya jumla ya kura zilizopigwa, tume imesema baadhi ya watu bado hawajapiga kura.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, Davidetta Browne-Lansanah, alisema barabara mbovu, mafuriko, na mvua ziliharibu baadhi ya vifaa vya uchaguzi na kuwazuiawatu kuwafika kwenye vituo vya kupigia kura katika baadhi ya wilaya.

"Vifaa vilivyoharibiwa vitabadilishwa kwa ajili ya kuendesha uchaguzi katika maeneo yaliyoathiriwa ndani ya wiki moja," alisema Browne-Lansanah.

"NEC itatuma timu kusaidia timu ya mahakimu katika kaunti haraka iwezekanavyo. Zaidi ya hayo, kushindwa kufika na ukosefu wa mtandao wa simu, hadi sasa hakuna taarifa za matokeo katika maeneo matano."

Tume ya uchaguzi inasema bila mawasiliano kutoka kwa maeneo hayo, hawawezi kubaini ikiwa upigaji kura huko ulifanyika au haukufanyika.

Mtandao wa waangalizi wa Uchaguzi nchini Liberia (LEON) umekuwa ukifuatilia uchaguzi huu, na kuitaka kamati ya uchaguzi kutoa maelezo zaidi kuhusu ukubwa wa maeneo ambayo bado hayajapiga kura.

Baadhi ya makundi ya waangalizi pia yaliwakosoa wafuasi wa vyama vya siasa wanaojitokeza barabarani kutangaza wagombea wao kuwa washindi, na kuwataka viongozi wao kuwa na subira kwa ajili ya matokeo rasmi.

Tume ya uchaguzi inasema zoezi la kuhesabu kura linaendelea na itatoa sasisho kila siku kusaidia kudhibiti matarajio na kuenea kwa uvumi.

Forum

XS
SM
MD
LG