Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:21

Muwaniaji urais Liberia Joseph Boakai azindua kampeni yake


Wanasiasa wa upinzani wa Liberia wahudhuria mkutano wa kampeni.
Wanasiasa wa upinzani wa Liberia wahudhuria mkutano wa kampeni.

Maelfu ya watu walikusanyika katika mji mkuu wa Liberia Monrovia siku ya Jumapili wakati kiongozi wa upinzani Joseph Boakai akizindua kampeni yake, kabla ya uchaguzi wa Oktoba, ambao utapima umaarufu wa nyota wa zamani wa kandanda George Weah, baada ya muhula wa kwanza uliogubikwa na utata.

Wafuasi wa Boakia, mwenye umri wa miaka 78, aliyeshika nafasi ya pili baada ya Weah. katika uchaguzi wa 2017, na ambaye amepewa jina la "Sleepy Joe" na wapinzani, kwa madai ya kulala kwenye hafla za hadhara, walistahimili mvua uwanjani, wakicheza densi na kupeperusha bendera huku wakidai mabadiliko.

Waliohudhuria ni baadhi ya mashabiki wa zamani wa Weah waliokatishwa tamaa na kile walisema ni kushindwa kwake kuboresha viwango vya maisha au kukomesha ufisadi katika nchi hiyo maskini ya Afrika Magharibi ambayo imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe karne hii, mlipuko mbaya wa Ebola, na kupanda kwa bei za bidhaa.

Forum

XS
SM
MD
LG