Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 11:02

Ikulu ya Niger imezingirwa - duru za usalama


Rais wa Niger Mohamed Bazoum alipokuwa Berlin Ujerumani, Julai 8, 2021. Picha na Bernd von Jutrczenka/Pool kupitia REUTERS.
Rais wa Niger Mohamed Bazoum alipokuwa Berlin Ujerumani, Julai 8, 2021. Picha na Bernd von Jutrczenka/Pool kupitia REUTERS.

Baadhi ya maafisa wa ulinzi wa rais wa Niger wamezingira ikulu ya rais katika mji mkuu Niamey, duru kadhaa za usalama zilisema Jumatano.

Ripota wa shirika la habari la Reuters aliona magari ya kijeshi yakifunga lango la ikulu ya rais. Ufikiaji wa wizara zilizo karibu na ikulu pia ulikuwa umezuiwa, vyanzo vya usalama vilisema.

Afisa mmoja katika afisi ya rais alisema wafanyakazi ndani ya ikulu hawangeweza kufikia afisi zao. Haikubainika mara moja ikiwa Rais Mohamed Bazoum alikuwa ndani.

Mji wa Niamey ulionekana kuwa mtulivu Jumatano asubuhi, huku usafiri wa barabarani ukiendelea kama kawaida, na huku kukiwa na ufikiaji kamili wa mtandao wa internet, ripota wa Reuters alisema.

Matukioa ya leo katika ikulu yanaleta kumbukumbu ya mapinduzi ya kijeshi ambayo yamezikumba nchi jirani za Mali na Burkina Faso tangu 2020.

Mapinduzi hayo yalichochewa, kwa kiasi, na mfadhaiko kutokana na kushindwa kwa mamlaka, kukomesha uasi wa Kiislamu unaoathiri eneo la Sahel, ambalo linajumuisha Niger.Pia kulikuwa na jaribio la mapinduzi lililokatizwa nchini Niger mnamo Machi 2021, wakati kikosi cha kijeshi kilipojaribu kuteka ikulu ya rais, siku chache kabla ya Bazoum, aliyekuwa amechaguliwa karibuni kuapishwa.

Niger ni mshirika mkuu wa madola ya Magharibi yanayotaka kuunga mkono wanajeshi wa ndani wanaopambana na uasi huo uliokita mizizi nchini Mali mwaka 2012 na kuenea katika nchi jirani zikiwemo Burkina Faso na nchi za pwani ya kusini mwa nchi hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG