Oparesheni ya siku 22 ambayo imemalizika Jumapili ililenga ngome ya kundi la Islamic State West Afrika (ISWAP), ya Arege kaskazini mashariki mwa mpaka wa Nigeria na Niger, jeshi limesema.
Magaidi hao 55 walio uwawa inajumuisha wanamgambo wa vyeo vya juu pamoja na viongozi wa kidini, taarifa imesema ikitumia neno la kiasili likimaanisha wanajihadi.
Takwimu zilitolewa katika mfumo wa mamwasiliano wa jeshi katika mkoa wa kusini mashariki wa Niger, Diffa shirika la habari la AFP iliona Jumatatu.
Oparesheni za aridhini na angani zilizolenga kutoa msukumo kwa kundi la ISWAP na kukata mawasiliano. Wanajeshi wawili waliuwawa na wengine watatu walijeruhiwa taarifa imesema.
Forum