Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:46

Watu zaidi ya 100 wamekufa maji katika ajali ya boti nchini Nigeria


Jamii ikishirikiana kutoa msaada kwa wahanga wa ajali ya boti katika jimbo la Kwara nchini Nigeria
Jamii ikishirikiana kutoa msaada kwa wahanga wa ajali ya boti katika jimbo la Kwara nchini Nigeria

Boti hiyo ilikuwa ikiwasafirisha watu katika jimbo la Kwara kutoka kwenye harusi katika jimbo jirani la Niger wakati ilipoanguka, polisi wa jimbo hilo na ofisi ya gavana walisema, bila kutoa maelezo ya chanzo cha ajali

Zaidi ya watu 100 wamekufa maji kaskazini mwa Nigeria baada ya boti iliyokuwa imebeba familia zilizokuwa zikirudi kutoka harusini kuzama katika mto, polisi na maafisa wa eneo hilo wamesema Jumanne.

Taarifa za kina kuhusu ajali hiyo iliyotokea katika jimbo la Kwara bado zinatolewa, lakini ni ajali ya hivi karibuni ya boti nchini Nigeria ambapo ni jambo la kawaida kutokana na boti hizo kupakia watu kupita kiasi, kukiuka taratibu za usalama na mafuriko makubwa katika msimu wa mvua.

Boti hiyo ilikuwa ikiwasafirisha watu katika jimbo la Kwara kutoka kwenye harusi katika jimbo jirani la Niger wakati ilipoanguka, polisi wa jimbo hilo na ofisi ya gavana walisema, bila kutoa maelezo ya chanzo cha ajali. Hadi sasa tuna watu 103 waliofariki na zaidi ya 100 wameokolewa kutokana na ajali ya boti, msemaji wa polisi wa jimbo la Kwara, Okasanmi Ajayi aliliambia shirika la habari la AFP kwa njia ya simu.

Utafutaji na uokoaji bado unaendelea na hii inamaanisha kuwa idadi ya watu huenda ikaongezeka. Ofisi ya gavana wa jimbo la Kwara haikutoa idadi ya watu, lakini ilisema waathiriwa walikuwa wakirudi kutoka kwenye sherehe ya harusi wakielekea wilaya ya Patigi katika jimbo la Kwara.

Forum

XS
SM
MD
LG