Shirika hilo lilisema kuwa uhaba wa fedha uliopo unamaanisha kwamba litaweza kusaidia takriban nusu ya watu milioni 11.6 waliolengwa, chini ya mpango wa dharura wa chakula, katika nchi, zikiwemo Burkina Faso, Nigeria na Chad, ambako wimbi la wakimbizi kutoka Sudan limekuwa shinikizo la ziada, kwa rasilimali chache zilizopo.
Migogoro na kupanda kwa bei za bidhaa kumechangia katika kuongezeka kwa uhaba wa chakula kwa miaka 10 katika maeneo ya Afrika Magharibi na Kati, kulingana na tathmini iliyofnaywa mwezi Machi mwaka huu na shirika la usalama wa chakula wa kikanda, Cadre Harmonise.
Kiwango cha utapiamlo pia kimeongezeka, huku watoto milioni 16.5, wa umri wa chini ya miaka mitano, wakitarajiwa kuwa na utapiamlo wa hali ya juu mwaka huu, WFP ilisema.
WFP inatafuta dola milioni 794 kujibu kushughulikia ipasavyo, mahitaji ya watu, katika nchi tano za kanda ya Sahel, zikiwemo Burkina Faso, Chad, Mali, Mauritania, na Niger kuanzia mwezi Julai hadi Disemba mwaka huu.
Forum