Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 11:56

Serikali ya Ethiopia na mashirika ya misaada wanahusishwa na kashfa ya udanganyifu; WFP


Miongoni mwa msaada wa vyakula uliopelekwa katika mkoa wa Afar huko Ethiopia. May 15, 2022.
Miongoni mwa msaada wa vyakula uliopelekwa katika mkoa wa Afar huko Ethiopia. May 15, 2022.

shirika la misaada ya kibinadamu la serikali ya Marekani, na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) walitangaza kuwa wanasitisha msaada wa chakula kwa eneo la Tigray lililokumbwa na vita nchini Ethiopia, baada ya kugundua kuwa shehena zilipelekwa katika masoko ya ndani

Viongozi katika serikali ya Ethiopia na mashirika ya misaada ya kibinadamu ni miongoni mwa washukiwa 186 wanaohusishwa na kashfa ya udanganyifu katika usambazaji, wa misaada ya chakula iliyokusudiwa kwa ajili ya kaskazini mwa nchi hiyo, tume ya uchunguzi ya Tigray imesema Alhamisi.

Mapema mwezi Mei, shirika la misaada ya kibinadamu la serikali ya Marekani, na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) walitangaza kuwa wanasitisha msaada wa chakula kwa eneo la Tigray lililokumbwa na vita nchini Ethiopia, baada ya kugundua kuwa shehena zilipelekwa katika masoko ya ndani.

Siku chache baadaye mashirika yote mawili yaliongeza uamuzi huo kwa Ethiopia nzima, huku USAID ikitaja kampeni iliyoenea na iliyoratibiwa ya kugeuza vifaa vilivyotolewa kutoka kwa wahitaji kama sababu ya kusimamishwa kwa shughuli hiyo.

Kulingana na Fiseha Kidanu, mkuu wa uchunguzi ulioanzishwa na mamlaka ya Tigray, mashirika matano ikiwemo serikali ya Eritrea, serikali ya Ethiopia, mamlaka ya mkoa wa Tigray, waratibu wa kambi za watu waliohamishwa na wafanyakazi wa misaada, walishiriki katika udanganyifu huo, vyombo vya habari rasmi viliripoti.

Forum

XS
SM
MD
LG