Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:56

Msaada wa chakula umesitishwa Ethiopia, msaada ulikuwa haufiki kwa walengwa


Mfanyakazi wa kutoa msaada akiwa anakagua magunia yenye chakula cha msaada kwa ajili ya watu wa Ethiopia.
Mfanyakazi wa kutoa msaada akiwa anakagua magunia yenye chakula cha msaada kwa ajili ya watu wa Ethiopia.

Shirika la chakula duniani WFP, limesitisha kwa muda utoaji wa msaada wa chakula kwa Ethiopia kwa sababu msaada unaotolewa haufikii watu wanaostahili kupata.

Tangazo la WFP limetolewa siku moja baada ya shirika la maendeleo la Marekani USAID kusema kwamba limechukua hatua ya kusitisha msaada wake kwa Ethiopia.

Mkurugenzi wa WFP Cindy McCain, ametaka serikali ya Ethiopia kuchunguza na kuwachukulia hatua wahusika katika Sakata hiyo.

Watu milioni 20 wanategemea msaada wa chakula nchini Ethiopia kutokana na vita na ukame wa muda mrefu.

Ethiopia ina jumla ya watu milioni 120 na kiwango kikubwa cha msaada kinatolewa na shirika la USAID na WFP.

Hakuna waliotajwa kuhusika na Sakata hiyo ya kuzuia chakula cha msaada kuwafikia watu wanaosthili, ambayo serikali ya Marekani inasema kwamba imeenea na inaonekana kupangwa kabisa.

Hata hivyo, barua iliyoandikwa na wafadhili wa nchi za nje inasema kwamba serikali inahusika na Sakata hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG