Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 05:36

Wanawake wachache kugombea kwenye uchaguzi wa bunge nchini Liberia


Rais wa Liberia George Weah
Rais wa Liberia George Weah

Tume ya uchaguzi nchini Liberia Alhamisi ilitangaza orodha ya awali ya wagombea kwenye uchaguzi wa bunge wa mwezi Oktoba, huku kukiwa asilimia 15 pekee ya wagombea wanawake licha ya juhudi za kupata asilimia 30 ya viti maalum bungeni.

159 tu kati ya watu 1,000 wagombea katika baraza la Seneti na baraza la wawakilishi ni wanawake, tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) ilitangaza.

Mwaka jana, wabunge walipitisha mswaada wa sheria unaovitaka vyama vya siasa kujumuisha si zaidi ya asilimia 70 na si chini ya asilimia 30 ya jinsia zote kwenye orodha ya wagombea wao, lakini Rais George Weah hakuusaini kuwa sheria.

Mwezi Mei, vyama vya siasa 25 kati ya 46 vilivyosajiliwa vilisaini makubaliano ya awali kwamba si chini ya asilimia 30 ya wagombea watakaoawapendekeza watakuwa wanawake.

“Wanawake watateseka tena na sauti zetu hazitasikika,” alisema Nora Neufville, afisa wa miradi katika shirika lisilo la kiserikali la wanawake la Liberia.

Amesema wamerudi nyuma.

Forum

XS
SM
MD
LG