Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 06:04

Mahakama ya umma ya The Hague imempata Putin na makosa ya uhalifu wa kivita


Rais wa Russia Vladimir Putin akihudhuria mojawapo ya sherehe ya kuweka maua kwa kaburi la mwanajeshi aliyeuawa mjini Moscow Feb 23, 2023
Rais wa Russia Vladimir Putin akihudhuria mojawapo ya sherehe ya kuweka maua kwa kaburi la mwanajeshi aliyeuawa mjini Moscow Feb 23, 2023

Mahakama ya umma, haina nguvu za kisheria, imempata na hatia rais wa Russia Vladimir Putin kwa makosa ya vita vya uhalifu dhidi ya Ukraine na kutaka akamatwe.

Uamuzi huo usio na nguvu zozote, umetolewa leo Ijumaa wakati ulimwengu unaadhimisha mwaka mmoja tangu Russia ilipoivamia Ukraine kijeshi.

Vikao vya mahakama ya umma (Peoples Court) vimefanyika wiki nzima mjini The Hague, na kusimamiwa na jopo la wataalam watatu wenye uzoefu mkubwa katika sheria za kimataifa.

Wameitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua kila hatua kuhakikisha kwamba mahakama yenye nguvu ya kisheria inatoa ilani ya kumtaka rais Vladimir Putin akamatwe haraka iwezekanavyo, pamoja na kuwachukulia hatua washirika wake katika vita hivyo na kufikishwa katika mahakama maalum kujibu mashtaka ya kuvamia Ukraine kijeshi.

Miongoni mwa majaji wa mahakama hiyo ni umma ni Stephen Rapp, mwendesha mashtaka wa Marekani ambaye aliongoza juhudi za kumkamata na kumfungulia mashtaka aliyekuwa rais wa Liberia Charles Taylor kwa makosa ya uhalifu dhidi ya Sierra Leone.

Mahakama imesikiliza ushahidi kutoka kwa waathirika wa vita vya Russia na wataalam wa kijeshi kabla ya kutoa uamuzi wao.

XS
SM
MD
LG