Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:04

Uchaguzi wa Liberia wafanyika Jumanne, Rais Weah akisema anatumaini kupata muhula mwingine


Rais wa Liberia George Weah akipiga kura yake Jumanne, mjini Monrovia.
Rais wa Liberia George Weah akipiga kura yake Jumanne, mjini Monrovia.

Rais wa Liberia George Weah anawania   muhula wa pili kwenye uchaguzi wa Jumanne, kwa matumaini  kwamba juhudi zake za kutengeneza barabara, kujenga hospitali na kusambaza umeme katika maeneo mengi zaidi zitamsadia kushinda.

Hilo ni licha ya matatizo ya uchumi yaliyopo kwenye taifa hilo la Afrika magharibi. Weah anakabiliana na washindani wengine 18 wakiongozwa na mpinzani wake mkuu kwenye uchaguzi wa 2017 Joseph Boakai, ambaye aliwahi kuwa makamu rais wakati wa utawala wa rais Ellen Johnson Sirleaf, aliyekuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia barani Afrika.

Weah analaumiwa kwa kutotimiza ahadi za kampeni kwamba angepambana na ufisadi, pamoja na kuhakikisha haki kwa waathirika wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyouwa takariban watu 250,000 kati ya 1989 na 2003. Wakati wa uchaguzi wa 2017, Weah alipata asilimia 61.5 ya kura zilizopigwa, Boakai akipata asilimia 38.5. Inasubiriwa kuona iwapo hali hiyo itajitokeza kwenye uchaguzi wa Jumanne. Wapiga kura milioni 2.47 wa Liberia pia wamepiga kura ya kuchagua wabunge kwenye zoezi hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG