Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 20:37

India: Mafuriko yasababisha vifo vya zaidi ya watu 70


Shughuli za uokoaji zinaendelea kufuatia mafuriko nchini India.
Shughuli za uokoaji zinaendelea kufuatia mafuriko nchini India.

Takriban watu 77 wamethibitishwa kufariki katika mafuriko yaliyokumba kaskazini mashariki mwa India, mamlaka zilisema Jumapili, na barabara na madaraja kuharibiwa na kuacha maelfu ya wengine bila uwezo wa kuvuka licha ya maji kupungua.

Mafuriko makubwa yalikumba jimbo la Sikkim siku ya Jumatano baada ya ziwa la barafu kupasuka ghafla.

Wanasayansi wanaonya kwamba majanga kama hayo yataendelea kuwa hatari inayoongezeka katika Milima ya Himalaya kadiri halijoto ya kimataifa inavyoongezeka na barafu kuyeyuka, ikichochewa na mabadiliko ya hali ya hewa.

"Jumla ya mili 29 imetolewa kutoka sehemu tofauti za Sikkim," kamishna wa misaada ya serikali Anilraj Rai aliliambia shirika la habari la AFP kwa njia ya simu.

Katika jimbo jirani la Bengal Magharibi, polisi wa wilaya ya Jalpaiguri waliambia AFP kwamba mili mingine 48 imepatikana.

Zaidi ya watu 100 bado hawajulikani walipo, kulingana na takwimu rasmi.

Afisa wa idara ya kudhibiti majanga ya jimbo la Sikkim aliiambia AFP kwamba zaidi ya watu 2,500 waliokuwa wamekwama kutokana na mafuriko hayo wameokolewa.

Lakini uhamishaji wa watu umekumbwa na changamoto kutokana na uharibifu wa barabara, madaraja na laini za simu katika sehemu kubwa ya Sikkim.

Forum

XS
SM
MD
LG