Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:18

Hali ya mivutano yajitokeza kuhusu ukarabati wa Derna, Libya baada ya mafuriko


Mji wa Derna, Libya ulioharibiwa na mafuriko Sept. 21, 2023.
Mji wa Derna, Libya ulioharibiwa na mafuriko Sept. 21, 2023.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Abdoulaye Bathily amesema Jumatatu kwamba ana wasi wasi kuhusu ushindani uliopo kati ya taasisi tofauti za Libya katika kukarabati mji wa Derna ambako mafuriko yaliuwa maelfu ya watu mwezi uliopita.

“ Juhudi zinazokinzana hazisaidii na zinaongeza migawanyiko iliyopo nchini, huku zikihujumu juhudi za ukarabati, kinyume na uungaji mkono na umoja wa kitaifa ulioonyeshwa na watu wa Libya,” amesema kupitia taarifa.

Libya imekuwa na serikali dhaifu tangu 2011 kufutia mapinduzi yaliongozwa na NATO, lakini ikagawanyika tena 2014 kati ya serikali iliyopo magharibi na nyingine upande wa mashariki. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters serikali ya mashariki ilisema kwamba imeahirisha kongamano na kimataifa lililokuwa lijadili ukarabati wa Derna.

Serikali inayotambuliwa kimataifa yenye makao yake makuu mjini Tripoli upande wa magharibi ilisema pia ilikuwa ikipanga mkutano wa kujadili kuhusu ukarabati wa Derna. Wachambuzi wanasema kwamba ukarabati wa Derna unaotarajiwa kuleta fedha nyingi kutoka mataifa ya kigeni huenda ukasababisha ghasia mpya kati ta serikali zote mbili.

Forum

XS
SM
MD
LG