Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 18:29

Utafiti wa uhamiaji wa hali ya hewa wazinduliwa Afrika


Timu ya utafutaji na uokoaji akitafuta miili ya watu kwa msaada wa mbwa, kufuatia mvua kubwa iliyosababisha mafuriko na maporomoko ya udongo huko na Durban, Afrika Kusini, Aprili 18, 2022. Picha na REUTERS/Rogan
Timu ya utafutaji na uokoaji akitafuta miili ya watu kwa msaada wa mbwa, kufuatia mvua kubwa iliyosababisha mafuriko na maporomoko ya udongo huko na Durban, Afrika Kusini, Aprili 18, 2022. Picha na REUTERS/Rogan

Wataalamu kutoka mataifa mbali mbali barani Afrika na kwingineko wamezindua utafiti kuhusu uhamaji wa hali ya hewa kote barani humo, huku mzungumzaji mmoja akionya kuwa kuna uwezekano wa watu milioni 86 huenda wakakoseshwa makazi ifikapo 2050.

Wawakilishi wa tume za ushauri katika mashirika ya ushauri wa kiuchumi ya Afrika katika mkutano unaofanyika katika mji mkuu wa Kinshasa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walisikia onyo kutoka kwa Ahmed Reda Chami katika hotuba yake kwa baraza hilo.

Kunaweza kuwa na "kuna uwezekano wa kuwa na wahamiaji wa ndani takriban milioni 86 ifikapo mwaka 2050 iwapo hakuna hatua zinazochukuliwa kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa," alisema Chami siku ya Jumanne.

Utafiti uliofanywa na Mabaraza ya Kiuchumi na Kijamii na Taasisi Sawa za Afrika (UCESA) unafadhiliwa na Benki ya Dunia, utajaribu kutazamia ukubwa wa matatizo kwa siku zijazo.

Reda Chami ni mkuu wa UCESA, ambayo ina wajumbe 19 wengi wao kutoka nchi zinazozungumza Kifaransa.

Mkutano mkuu wa UCESA ulianza mjini Kinshasa siku ya Jumanne, Pia kuhudhuriwa na wajumbe kutoka taasisi kama hizo zilizoko Ulaya na China.

"Hatima ya ubinadamu inaangaliwa," alisema Jean-Pierre Kiwakana, rais wa baraza la kiuchumi na kijamii la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wataalamu wanadai kuwa Afrika inakabiliwa na hatari kubwa zinazohusishwa na ongezeko la joto duniani, na ongezeko la viwango vya juu vya joto na uhaba wa mvua ambao umesababisha maafa katika nchi maskini.

Kwa mfano, mafuriko makubwa katika nchi iliyokumbwa na vita, Libya mwezi huu yaliua zaidi ya watu 3,800, kulingana na takwimu rasmi, na maelfu ya watu kuyahama makazi yao.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG