Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva mkurugenzi mkuu wa WMO Peterri Taalas amesema changamoto kubwa za Libya ni kumudu hali baada ya mafuriko ambayo yameuwa maelfu ya watu na kwamba uongozi haufanyi kazi ipasavyo.
Petteri Taalas, mkurugenzi mkuu wa WMO anasema: “Ndio, hilo ndiyo hitimisho , kama kungekuwa na idara ya huduma ya hali ya hewa ingakuwa inafanya kazi kama kawaida, wangeweza kutoa maonyo na pia mamlaka za dharura zingeweza kuokoa watu na tungeepuka majeruhi wengi.
Huduma za uokozi zinakuwa ngumu kutokana na mgawanyiko wa kisiasa katika nchi hiyo yenye takriban watu milioni saba.
Watu hao wamekuwa katika vita mara kadhaa bila kuwa na serikali kuu iliyo imara tangu NATO ilipounga mkono kuondolewa madarakani Muammar Gaddafi mwaka 2011.
Forum