Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:59

Watu 30,000 wakosa makazi Libya


Taasisi ya kimataifa ya uhamiaji Jumatano imesema mafuriko mabaya ya mashariki mwa Libya yamesababisha watu zaidi ya 30,000 kukosa makazi

Idara hiyo ya Umoja wa Mataifa imesema takribani watu 30,000 wamekoseshwa makazi wanatokea mji wa Derna huku maelfu zaidi wakitokea maeneo mengine ikijumuisha Benghazi.

Zaidi ya watu 5,000 wanaaminika kupoteza maisha huku idadi kamili ikiwa ni ngumu kuthibitisha katika taifa hilo ambapo serikali zinazo kinzana zimekuwa zikipigania kuchukua udhibiti kamili kwa muongo mmoja sasa.

Baadhi ya maafisa wanasema idadi hiyo inaweza kuwa mara mbili. Waziri wa usafiri wa anga wa kiraia Jichem Abu Chkiouat, wa utawala unaoongoza upande wa mashariki, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba zaidi ya miili 5,300 imehesabiwa katika eneo la Derna.

Forum

XS
SM
MD
LG