Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 05:46

Zaidi ya watu 43,000 wamehamishwa kwenye makazi yao na mafuriko katika mji wa Libya wa Derna-IOM


Picha hii inaonyesha wakoaji wa Misri wakiendelea kutafuta miili baada ya mafuriko yaliyoukumba mji wa Libya wa Derna, Septemba 21, 2023.
Picha hii inaonyesha wakoaji wa Misri wakiendelea kutafuta miili baada ya mafuriko yaliyoukumba mji wa Libya wa Derna, Septemba 21, 2023.

Mafuriko ya Libya ambayo yaliua maelfu ya watu katika mji wa Derna, yamewahamisha pia kwenye makazi yao zaidi ya watu 43,000, shirika la kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema Alhamisi.

Mafuriko makubwa yenye ukubwa wa tsunami yalipita kwenye mabwawa mawili yaliyozeeka juu ya mto wa mji huo baada ya mvua kubwa kunyesha katika mji huo tarehe 10 Septemba.

Yaliteketeza vitongoji vyote na kusomba maelfu ya watu kwenye bahari ya Mediterania.

Idadi rasmi ya vifo bado ni zaidi ya 3,300, lakini idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka, huku mashirika ya kimataifa ya misaada yakikadiria kuwa hadi watu 10,000 hawajulikani walipo.

“Takriban watu 43,059 walihamishwa kwenye makazi yao na mafuriko kaskazini mashariki mwa Libya,” IOM imesema, na kuongeza kuwa “ukosefu wa maji unaripotiwa kusababisha watu wengi waliohamishwa kwenye makazi yao kuondoka Derna” na kuelekea maeneo mengine.

IOM imesema mahitaji ya haraka ni pamoja na chakula, maji ya kunywa na huduma ya afya ya akili na kisakiolojia.

Huduma za simu za mkononi na intaneti zimerejeshwa leo Alhamisi baada ya kusitishwa kwa siku mbili, kufuatia maandamano ya siku ya Jumatatu ambapo wakazi wenye hasira walilaumu mamlaka kwa idadi kubwa ya vifo.

Forum

XS
SM
MD
LG