Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 01:37

Masuala ya siasa, uchumi na mabadiliko ya hali ya hewa kujitokeza katika Mkutano wa Baraza Kuu la UN


Ukumbi ambapo mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa utafanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani.
Ukumbi ambapo mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa utafanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani.

Vita nchini Ukraine huenda likawa suala kubwa kwa mwaka wa pili mfululizo wakati viongozi watakapokusanyika katika mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa huko New York wiki ijayo.

Lakini nchi nyingi zinazoendelea zina matumaini ya kuangaziwa kwa masuala muhimu kwao, ikiwa ni pamoja na maendeleo, mfumuko wa bei na mabadiliko ya hali ya hewa.

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa mwaka huu litafanyika baada ya mikutano kadhaa, na baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu hawatahudhuria mkusanyiko huo wa kila mwaka. Lakini bado kuna mengi ya kuzungumza kuhusu mkusanyiko huo.

“Tutakusanyika wakati ambapo ubinadamu unakabiliwa na changamoto kubwa – kuanzia dharura mbaya ya hali ya hewa mpaka kusambaa kwa mizozo, mzozo wa kupanda kwa gharama za maisha ulimwenguni, kuongezeka kwa ukosefu wa usawa, na usumbufu mkubwa wa teknolojia. Watu wanawaangalia viongozi wao kubuni ya kuondokana na hali hii,” Antonio Guterres anasema.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy anatarajiwa kuhudhuria binafsi, kwa mara ya kwanza tangu Russia iivamie nchi yake Februari 2022. Ni fursa kwake kuomba msaada wa kimataifa, lakini lazima pia atembee katika njia nyembamba ya kidiplomasia.

Volodymyr Zelenskyy
Volodymyr Zelenskyy

Richard Gowan, Mkurugenzi wa International Crisis Group anasema, “Zelenskyy inamlazimu awe makini kwamba kuna viongozi wengikutoka nchi zinazoendelea, ambao wana matatizo yao wenyewe—kama vile madeni na ukuaji mbaya wa uchumi – na wanataka kuzungumza kuhusu masuala hayo, na siyo tu vita kati ya Russia na Ukraine.”

Hiyo inajumuisha maendeleo endelevu, ambayo hayako kwenye mwelekeo wa kutimiza malengo ifikapo mwaka 2030 ili kumaliza njaa na umaskini uliokithiri. Umoja wa Mataifa unasema kama mwenendo wa sasa utaendelea, takribani watu milioni 575 watabaki wamekwama katika umaskini uliokithiri ifikapo mwisho wa muongo huu.

Mkutano wa siku mbili ambao Umoja wa Mataifa una matumaini utafufua malengo utaanza na mikutano ya ngazi ya juu.

Astra Bonini, Afisa Mwandamizi wa UN wa Maendeleo Endelevu anazungumzia kuhusu maendeleo. “Maendeleo yamerudi nyuma sana katika miaka ya karibuni. Hii kwa kiasi inatokana na kuwepo kwa janga la Covid 19, kiwango cha juu cha mizozoya silaha ulimwenguni tangu mwaka 1945, na majanga yanayohusiana na hali ya hewa, pamoja na mfumuko wa bei na kupanda kwa gharama za maisha.”

Pia kutakuwepo na mazungumzo kuhusu hali ya hewa siku ya Jumatano ambapo nchi zitahitaji nia ya dhati ya kupunguza gesi chafu na awamu ya mafuta mbadala kwa viongozi kuelezea kwenye majukwaa.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia litakutana siku hiyo kwa majadiliano ya ngazi ya juu kuhusu vita nchini Ukraine. Rais Zelenskyy anatarajiwa kuhudhuria.

Katibu Mkuu anasema kuna nafasi ya kujadili yote vita nchini Ukraine na masuala mengine mazito katika wiki hiyo. Amesema ‘kuokoa’ Malengo ya Maendeleo Endelevu ni sualmuhimu.

Antonio Guterres anasema “naamini kwamba kuna nafasi kwa masuala yote kujadiliwa kwa dhati, na sikhofii kwamba kuna mizozo tofauti ambayo tunaishuhudia katika sehemu tofauti za dunia, kwamba watachukua agenda ya umuhimu wa SDGs.”

Rais Joe Biden atalihutubia baraza kuu siku ya Jumanne asubuhi, akiweka kipaumbele cha Marekani.

Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

“Atahutubia katika Baraza Kuu, ambako atathibitisha tena uongozi wa nchi yetu katika kukabiliana na vitisho kwa amani na usalama wa kimataifa, kulinda haki za binadamu, na kusukuma ustawi na maendeleo ya ulimwengu,” anasema balozi Thomas-Greenfield

Huku kukiwa na mambo mengi, raia wa dunia watawaangalia viongozi kama wanaweza kuchukua hatua kuboresha maisha yao ya kila siku na kulinda mustakbali wao.

Ripoti na Mwandishi Margaret Besheer wa VOA

Forum

XS
SM
MD
LG